BALOZI WA AIRTEL TANZANIA 'AY' AWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA VIFAA VYA KUFUNDISHIA KATIKA SHULE YA VIZIWI.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Press Release
Ni moja kati
ya shule zitakazofaidika na mradi wa Airtel na BAMVITA
Wanafunzi wa shule ya Buruguni viziwi wameomba watanzania na wadau mbalimbali
kuchangia ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo
mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa
kushirikiana na BAMVITA. Wanafunzi hao waliosema hayo wakati Airtel pamoja na
balozi wake AY walipotembelea shuleni hapo mwisho mwa wiki hii.
Wanafunzi wa shule ya buruguni viziwi ambao mbali na masomo
ya darasani pia wanafundishwa kazi za stadi, walionekana kufanya kazi za stadi
za mikono ikiwemo kutengeneza shanga pamoja na mazulia madogo ya miguu, wametia
hamasa na kuthibithisha kwamba
wakiwezeshwa na kupatiwa nyenzo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya
shughuli za stadi na ubunifu.
Akiongea katika ziara hiyo Meneja huduma za jamii wa Airtel
Hawa Bayumi alisema “leo tumetembelea shuleni hapa ikiwa ni mwendelezo wa
utaratibu wetu katika kubainisha mahitaji ya ziada ambazo shule hizi zenye
mahitaji maalumu zinahitaji. Shule ya Buruguni viziwi ni moja kati ya shule
zitakazofaidika Mradi huu unaoshirikisha Airtel na BAMVITA una lengo la
kusaidia kuendeleza kiwango cha Elimu hapa nchini na kutoa nafasi kwa jamii
yetu kuweza kushiriki na kuchangi elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji
maalum."
Naye Balozi wa Airtel AY Ambwene Yesaya alisema “
Tunawashukuru watanzania kwa kuitikia wito na kuanza kuchanga na tunaendelea
kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda
namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi
200 au kuchangi kiwango chochote kupitia Airtel money 0788 041361 ambapo jina
la fumbo ni VITABU.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi bi. Winfrid
Jeromia alikuwa na haya ya kusema” tunaishukuru sana
Airtel kwa kuweza kuja na mradi kama huu wa
kuweza kuinua Elimu hapa nchini na kurahisha mazingira yetu ya ufundishaji hapa
shuleni. Tunawaomba watanzania wengine na makampuni mengine makubwa yajitokeze
kwa wingi kuweza kuchangia katika mradi huu ili kuinua wigo wa Elimu hapa
nchini.
Kampeni hii ya kuchangia vifaa kwa shule zenye mahitaji
maalumu inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana ilizinduliwa Agosti 23 2012 na
itaendelea kwa muda kwa mienzi mitatu. Kwa kuanzia shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni
Uhuru Mchanganyiko, Sinza Maalum, na Buguruni Viziwi zitafaidiaka na mradi huu.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA