Header Ads

Breaking News
recent

JINSI YA KUEPUKA MADENI NA KERO ZA KUDAIWA KWA MUDA MREFU.

HUENDA ukawa  unadaiwa madeni mengi na unaona nivigumu kwako kukabiliana nayo moja kwa moja, usiogope jaribu njia mbadala za kuweza kukabiliana na madeni hapa.Zifuatazo ni baadhi ya njia zitakazo kusaidia kupambana na ulipaji wa madeni .

1: Tengeneza Orodha yote ya madeni unayodaiwa.

    Unapaswa kufahamu madeni yote unayodaiwa na umjue mtu, kikundi au kampuni inayokudai.Kufanya hivyo kutakukumbusha kujipanga vizuri katika swala zima la ulipaji.

2: Panga madeni yako kulingana na kiasi, umuhimu na uharaka wa kuyalipa.

    Yapatie kipau mbele yale madeni uhimu yanayoweza kukuchukulia hatua mara moja.Mara nyingi madeni haya huwa ni ya kawaida, kwa mfano; kodi ya nyumba, kusimamishiwa huduma muhimu(maji, umeme) Ada ya shule au hata kwenda jela.Lakini sii lazima uanze tu na madeni ya aina hii, bali inategemeana na hali iliyopo.

3:  Tengeneza bajeti yako peke yako.

     Fanya mahesabu ili kujua kipato ulichoingiza kwa wiki au mwezi, pamoja na gharama zake zote, hii itakusaidia sana kuokoa pesa zako.Bajeti itakusaidia kuamua nini unaweza kumudu kulipa wadai wako, hivyo ni muhimu kuwa mkweli.

4: Kuwa mkweli na muwazi kwa wadeni wako.

    Watu wengi wanafikili kumkwepa mdeni wake ndiyo njia pekee ya kukabiliana na madeni, hapana! mara nyingi hii hukujengea taswira mbaya katika jamii unayoishi nayo.Nivyema ukapokea simu ya mdeni wako na kumwambia ukweli na kuomba akuongezee muda wa kuweza kujipanga zaidi na kufanikisha kulipa madeni yako.

5: Tumia njia ya mazungumzo baina yako na mtu anaye kudai.

    Nivyema ukakubaliana na mdeni wako kias na jinsi ya kulipa deni, nakama ikishindikana baadaya kuwa umeshakopa, tafuta ushauri kwa wataalam, watakusaidia jinsi ya kulipa madeni, kwa mfano taasisi binafsi zinazohusika na mikopo katika jamii.Nivyema ukakabiliana na madeni yako moja kwa moja- kwasababu jinsi upuuzavyo kulipa madeni ndivyo hali itakavyozidi kuwa mbaya kwako.

NB
 Kamwe usikimbie madeni, jitahidi ukabiliane na madeni kwa kutumia lugha nzuri kwa mdeni wako, kwasababu madeni humkosesha mtu uhuru, amani na hata pia huhatarisha maisha.Asante!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.