Header Ads

Breaking News
recent

MWANDISHI MKONGWE WA IKULU YA MAREKANI "HELEN THOMAS" AFARIKI DUNIA.

Mwandishi mkongwe wa Ikulu ya Marekani (white house) Helen Thomas afariki dunia Julai 20/ 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.Add caption
Kwa mujibu wa CNN, Heleni amefariki akiwa na umri wa miaka 92 ikiwa ni baada ya kuugua kwa kipindi kirefu. Helen amefanya kazi na marais wa Marekani wapatao 10 ikiwa ni takribani nusu karne.

Kutokana na kuwa mahiri katika kazi na kwa muda mrefu, Helen alikuwa ni kiongozi katika mikutano ya habari maelezo ya Ikulu ya Marekani, ambapo alikuwa akiwachapa marais maswali moto moto.

Naye Rais Barack Obama ameeleza ujumbe huu baada ya kifo cha mwandishi huyu mkongwe "not just the length of her tenure, but her fierce belief that our democracy works best when we ask tough questions and hold our leaders to account,"
Na hapa Helen alikuwa akimuhoji swali rais
Ronald Reagan wakati wa habari maelezo katika Ikulu ya Marekani (White House) mnamo March 19,1987.

Pia bibi huyu alianza kazi ya uandishi ndani ya Ikulu ya Marekani tokea kipindi cha rais John F. Kennedy mwaka 1961 hadi alipostaafu mnamo mwaka 2010.

Kwa mujibu wa CNN, taratibu za mazishi zinaendelea.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.