Header Ads

Breaking News
recent

KOCHA WA KIMATAIFA KATIKA MCHEZO WA RIADHA NCHINI "SAMWEL TUPPA" AKIWA MAZOEZINI NA WASHINDI WA MEDALI KITAIFA

Kocha wa mchezo wa riadha bw. Samwel Tuppa akiwa katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha wakati akiwafanyisha  mazoezi ya kuruka washindi wa medali za mchezo wa huo kitaifa.

Kocha Tuppa akiongea na ASILI YETU TANZANIA amesema kuwa yuko katika harakati za kuwanoa vijana wake ili hivi karibuni waweze kuungana na timu ya Taifa ya mchezo huo katika michezo ya kitaifa itakayokuwa ikifanyika hivi karibuni.

Huyu ni mshindi wa kitaifa wa medali nne, akiwa katika mazoezi na kocha wake Samwel Tuppa katika uwanja wa makumbusho ya hayati Karume mjini Arusha.

Tupa emeleza changamoto nyingi zinazowakabili wachezaji wake, yakwanza ikiwa ni wadhami kutojitokeza kuwaunga mkono katika kuwawezesha kukidhi mahitaji ya vifaa mbali mbali  vya mazoezi na kuwasaidia kushiriki mashindano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.


Ni wito kwa watanzania kujitokeza kuwawezesha wachezaji hawa na washindi wa medali za mchezo wa kuruka nchini, kwani wanauwezo mkubwa wa kushiriki na kunyakua medali zaidi ya hizo nje ya nchi na kuweza kuitangaza Tanzania kimataifa.

Mshindi wa kitaifa wa medali nne katika mchezo wa kuruka, akiwa katika mazoezi ya mchezo huo katika uwanja wa Karume jijini Arusha.



No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.