KABATI ALLSTARS - IRINGA BILA UKIMWI INAWEZEKANA (NEW SONG).
Kibao hicho alichorekodi na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya walioibuka washindi wa shindano hilo la kusaka vipaji, umerekodiwa katika studio za Top Magic Sound chini ya mtayarishaji wake mahiri Ecko Wimbo huo ni harakati za mbunge Kabati alizozianzisha katika kuwakomboa vijana katika majanga na makundi hatarishi kama ya uvutaji wa bangi, ngono zembe zinazochangia maambukizi ya ukimwi - Ugonjwa ambao kwa mujibu wa takwimu za mkoa huu unaongoza kwa maambukizi mapya.
Akizungumzia wimbo huo, Kabati amesema kuwa anaimani ujumbe uliomo utaifanya jamii kubadilika na hatimae kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi mkoani Iringa na Taifa kwa ujumla.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA