Shirika la Fedha Duniani 'IMF' limeonesha hali ya Uchumi Afrika.
Shirika la Fedha Duniani IMF limetoa
ripoti yake kuhusu hali ya ukuaji wa uchumi katika nchi za eneo la chini
ya jangwa la Sahara barani Afrika ambapo inaonesha kuwa Uchumi
unatazamiwa kupungua kwa kiasi kikubwa ambacho hakijawahi kushuhudiwa
katika kipindi cha miaka 20.
Ripoti
ya IMF imesema uchumi katika eneo hilo unatazamiwa kustawi kwa kiwango
cha asilimia 1.5 mwaka huu, kutokana na mfumko wa bei za bidhaa sambamba
na mazingira mabaya ya kiuchumi duniani.
Hata hivyo
ripoti hiyo imebainisha kuwa, uchumi wa nchi kama Kenya, Ethiopia,
Ivory Coast na Senegal ambazo hazina maliasili, zinafanya vizuri
kutokana na marekebisho katika sekta ya miundombinu na vile vile kuagiza
mafuta kwa bei ya chini.
Aidha ripoti
ya IMF imesema kuwa, Uchumi wa nchi zinazoagiza bidhaa kama Angola,
Nigeria na Afrika Kusini unayumba kutokana na kuporomoko kwa bei ya
mafuta katika masoko ya kimataifa.
IMF
imezitaka nchi za eneo la chini ya jangwa la Sahara kufanya marekebisho
katika sekta za kijamii, kimuundo na kwenye hazina ya serikali ili
kutoshuhudia ukuaji mdogo wa uchumi wao.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA